Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe ameiomba serikali kupitia
Bunge lake la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuacha kufanya kazi kwa
matakwa ya watanzania wachache na kuwaacha watazania wengi ambao ni
walipa kodi kwenye matatizo.
Ameyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na East Africa
Radio wakati akifafanua kile kinachoendelea kwa sasa Bungeni na kuwaomba
wabunge wenzake kuhakikisha wanasimamia haki ya kikatiba katika
kutafuta maendeleo ya nchi na kuongeza pato la taifa.
Amesema kuwa watanzania wengi wanategemea wawakilishi wao ambao ni
wabunge waliowachagua kidemokrasia kuwafikishia matatizo yao serikali
kupitia Bunge kwa lengo la kuwasaidia na kuyatatua matatizo yao ndani ya jamii zao.
Aidha Mhe. Zitto amesema kuwa haipaswi bunge kubanwa kitu ambacho
kitaminya demokrasia, hivyo ni vyema bunge likaachiwa huru lifanye kazi
yake ya kuisimamia serikeli kama sheria na kanuni inavyotaka.

0 comments:
Post a Comment