Kocha ambaye bado anatajwa kuwa siku zake zinahesabika kuendelea kusalia ndani ya Man United Louis van Gaal, amerudi kwenye headlines na kauli ambayo huenda imewashangaza wengi. Louis van Gaal
amekuwa akikosolewa na wachambuzi wa masuala ya soka Uingereza pamoja
na wachezaji wa zamani wa timu hiyo juu ya mfumo wanaocheza Man United kwa sasa.
Kumbe sio mashabiki na wachambuzi wa soka pekee ndio huwa wanaumizwa na namna Man United wanavyocheza soka kwa sasa, bali hata Louis van Gaal ambaye ni kocha wa timu amekiri kuboreka wakati mwingine kuona Man United ikicheza mchezo mzuri, Van Gaal anakiri kuwa zipo mechi za Man United ambazo huwa anafurahia na zipo ambazo huwa zina mkera na kumtia hasira.
“Kuna
baadhi ya mechi za Man United huwa na furahia sana kuona namna ambavyo
timu inacheza, mfano mechi yetu ya karibuni tuliyocheza dhidi ya
Chelsea, ila kuna baadhi ya mechi huwa napata hasira sana, lakini hilo
ndio soka lilivyo sio kila siku timu itacheza mpira mzuri"
source; millardayo.com
source; millardayo.com

0 comments:
Post a Comment