Mapenzi Salama Na Njia Za Kuzuia Mimba

Mapenzi salama

Kama unahisi uko tayari kufanya mapenzi, au tayari unashiriki katika ngono, ni vyema kuchukua tahadhari. Hakikisha katika harakati zako za kufanya mapenzi, unajali afya yako kwa kufanya ngono iliyo salama. 

Inaweza kuwa vigumu, na jambo unalolionea haya kujadiliana na mapenzi wako, swala la uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa, na kutumia njia za kuzuia mimba.
Lakini kulikwepa swala hilo kwaweza kumaanisha kuhatarisha afya na maisha yako kwa jumla. Kufanya mapenzi salama , maana yake ni kutafakhari maswala hayo na kisha kuchukua hatua zifaazo.

Punyeto Ni nini?

Kufanya au kupiga punyeto, ni tendo la kutomasa sehemu zako mwenyewe za siri ili kujisisimua kimapenzi.
Kwa hivyo katika kupiga punyeto hamna hofu ya kuambukizwa magonjwa yanayosambazwa kupitia ngono, kwani haimshirikishi mtu mwengine.
Punyeto ni toshelezo kamili la kimapenzi kama utatumia njia mbali mbali za kujitomosa na kujipa papasa ya kujistarehesha.
Hakuna mtu anayezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inakubidi kujifunza kwa majaribio salama.
Na, kwa vile kila mtu yuko tofauti, njia nyengine ya kujua jinsi unavyoweza kumstarehesha mpenzi wako, ni kujifunza kutoka kwako mwenyewe.
Shughulika zaidi na sehemu ambazo zinasisimka kwa urahisi.
Unaweza kufikia kilele cha starehe yako kwa kuitomasa tomasa mboo au kisimi, lakini kutakupa hamu kubwa na ashiki, na kufikia kutoshelezwa vya kutosha, kama utapapasa pia sehemu nyenginezo za mwili wako.
Kwa nini punyeto huonekana kuwa makosa?
Msimamo wa dini nyingi na watu wengi ni kuwa punyeto ni dhambi, mwiko, jambo lililokatazwa, jambo lisilokubalika kabisa.
Lakini wanasanyansi wanasema ni jambo salama kiafya na dhana zilizopo kulihusu, ni imani za kibinafsi na chaguo la mtu.
Wanaume wengi na wanawake hupiga punyeto maishani mwao, kwa sababu huwafanya wakajisikia vizuri na huondoa dhiki za mihemko ya kimapenzi bila kujiingiza katika ngono na mtu mwengine.
Pia hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo virusi vya HIV ni kichocheo tosha kinachopelekea baadhi ya watu kupiga punyeto.

Njia za kuzuia mimba

Dawa au vifaa vya uzazi ni baadhi ya taratibu zinazotumiwa kuzuia mimba kutungwa. Ikiwa msichana au wanamke atafanya mapenzi pasi na kutumia mojawapo ya mbinu hizo basi, kuna uwezekano wa theluthi moja kwamba atapata mimba.
Hata hivyo aina yoyote ya kuzuia mimba utakayoichagua ni lazima itumiwe kama ilivyoagizwa, ili kuleta matokeo ya hakika.
Baadhi ya njia hizo kama vile kutumia kondom wakati wa ngono, pia kwa kiasi fulani humpa mtu kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya HIV, na magonjwa mengine yanayoathiri afya ya uzazi.
Kwa vile mbinu za kuzuia uzazi ni za aina tofauti tofauti, ni muhimu basi uchague kwa makini ile inayokufaa. Utapata usaidizi wa kitaalam kama utashauriana na daktari wako, au pata usaidizi katika kituo cha kwenu cha upangaji uzazi, au kituo cha vijana.
Mbinu za kuzuia mimba (Contraception)
Hivi ni vifaa au dawa zinazotumiwa kwa minajili ya kuzuia mimba kutungwa wakati wa kufanya ngono.
Kuna zile zinazotumiwa kwa mda mfupi na nyengine kwa mda mrefu. Nyengine hufanya kazi papo hapo na nyengine huitaji maandalizi ya mda.
Kondom au tembe maalum ndizo njia bora zinazojulikana zaidi za kuzuia mimba.
Pia kondom zina manufaa bora zaidi zinapotumuwa kwani mbali na kuzuia mimba zinapotumika kama inavyopaswa zinaweza pia kumkinga mtu asiambukizwe vurusi vya HIV, na magonjwa mengine ya zinaa.

Tuangalie kwanza vifaa vya kuzuia mimba.



Moja ya mbinu bora na rahisi za kuzuia mimba, ni kuweka kizuizi, kwa lengo kuwa mbegu ya mwaname na ile mwanamke zisikutane. Kwa maana hiyo kifaa maalum kinaweza kuwekwa katika njia inayotumiwa na mbegu ya kiume ndio isilifikie yai la mwanamke.
Baadhi ya vifaa hivi (hasa kondom) pia vinaweza kukinga kuambukizwa virusi vya Ukimwi, na magonjwa mengine ya kuambukizana kupitia ngono.
Kuna aina kadhaa za vifaa vya kuzuia mimba. Kondom za wanaume na zile za wanawake ndio vifaa vinavyofahamika zaidi, hata hivyo kuna pia vifaa vyenginevyo viitwavyo diaphragm na caps kwa kimombo ambavyo vinaweza kutumiwa na wanawake.
Kondom za wanaume: Hivi hutengenezwa kutokana na aina maalum ya mpira uitwao latex, au plastiki nyembamba. Kondom ya mwanaume huvaliwa kwenye uume iliyosimama, tena kabla ya uume kuingizwa ukeni. Ikitumiwa kama inavyotakikana inakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98.
Kwa kawaida kondomu hupatikana kwenye vituo au kliniki za upangaji uzazi, kwenye maduka ya madawa au hata maduka ya kawaida.
Kondomu za wanawake: Halkadhalika hutengenezwa kwa mipira laini ya latex au plastiki nyembamba maalum. Huvaliwa ndani ya uke, huku sehemu iliyowazi ikichomoza nje kidogo. Kwa kawaida kondom za wanawake ni ghali, na pia utendaji kazi wake unakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 95.

Aina nyenginezo na vifaa vya kuzuia mimba huwa hazipendekezwi kwa vijana lakini ni vyema kuvijua.

Kuna aina nyenginezo za vifaa vya kuzuia mimba viitwavyo diaphragms na caps. Hivi hutengenezwa kutokana na kitu kiitwacho silicone au mpira laini maalum. Vikiwekwa ukeni hutumika kama vizibo vya kuzuia mbegu za mwanamme kupenya hivyo basi haiwezi kukutana na yai la mwanamke.
Kwa kawaida caps ni ndogo kuliko diaphragms lakini kwa vile wanawake pia wana maumbo tofauti, ni sharti upate saizi utakayokutosha. Hapa ni sharti upate usaidizi wa daktari wako, au muuguzi, kuiweka.
Inapowekwa mahali pake ndani ya uke, iwe diaphragm au cap, huziba kilango cha mfuko wa uzazi hivyo basi mbegu ya mwanamme haitapatanafasi ya kupita. Ukishaonyeshwa na daktari jinsi ya kuipachika, baadae unaweza kuipachika mwenyewe kabla ya kufanya mapenzi.
Kwa matokeo bora zaidi, diaphragms na caps hutumiwa pamoja na dawa iitwayo (spermicide) ambayo huuwa mbegu za uzazi za mwaname. Hapo diaphragms au caps humpa mwanamke kinga dhidi ya mimba kwa asilimia kati ya 92 na 98.
Hata hivyo itachukua mazoezi ya muda ili kuvitumia itakikanavyo. Wakati mwengine pia hutumiwa na gel yake maalum lakini bado havina hakikisho la asilimia moja kuzuia mimba.
Faida yake nyengine ni kuwa, kwa kiasi fulani, vinaweza kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na saratani ya (cervix) lango la nyumba ya uzazi.
Ikiwa wewe hutumia vifaa kama diaphragms au caps, au hata kondom, ni vyema kujipangia mapema ndio usikose akiba, ndio haitakuwa karaha kuvitafuta pale unapovihitaji. 

ITAENDELEA........
Source; www.bbc.com
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment