Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona Neymer akiwa katika pozi.
Kikosi cha XI bora cha FIFA Messi akisalimiana na Samuel Etoo

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Barcelona, na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ametwaa tuzo ya mchezo bora wa dunia.
Messi mwenye miaka 28 alishinda kwa 41.33% kwa kura zote zilizopigwa,
huku Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya pili kwa 27.76% na Neymer
akipata 7.86%.
Hii ni mara yake ya tano kutwaa tuzo hiyo.
Kwa upande wa wanawake nyota wa Marekani Carli Lloyd, ameibuka kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake.
Goli bora la mwaka likifahamika kama Puskas limwendea Wendell Lira anayekipiga katika Atletico Goianiense ya Brazil.
Kocha wa Barcelona Muhispania Luis Enrique amechaguliwa kuwa kocha
bora wa mwaka kwa kuiongoza barca kufanya vizuri barani Ulaya kwa kutwa
mataji matano msimu uliopita.
Jill Ellis kocha wa kikosi cha taifa cha Marekani amekuwa kocha bora
wa wanawake baada ya kuongoza timu ya taifa ya Marekani kufanya vyema
katika michuano ya kombe la dunia.

0 comments:
Post a Comment