Paul na Peter, P-Square.
KUNDI la muziki linaloundwa na pacha wawili, Paul na Peter, P-Square
huenda linaenda kusambaratika kama inavyoendelea kuanikwa na mashabiki
wao.
Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu mmoja wa wanaounda kundi hilo, Peter
kufanya kazi kivyake, kumiliki kampuni yake na kutengeneza kipindi
chake kiitwacho Dance With Peters maswali mengi yamekuwa yakiibuka na
kuuliza kulikoni kwa Paul.
Hivi karibuni, Paul naye ameibuka kivyake na kufanya kazi kivyake
ambapo kwa sasa anamiliki kampuni yake ya kurekodia muziki iitwayo
Rudeboy Records na kizuri zaidi tayari ameshamsainisha msanii mmoja
aitwaye, Muno Sings na wamekuwa karibu kama alivyo Daimond kwa msanii
wake Harmonize.

Katika kuufungua mwaka, Paul aliwaambia mashabiki wake;
“2016, Muno Sings. Mashabiki wangu kaeni mkao wa kusikia sauti ambayo haijawahi kutokea. Nakuja. Rudeboy Records inaendelea.”
Kisha Paul akasisitiza kwamba hajafanya makosa kabisa katika kuandika
jina la Lebo ya Rubeboy na baada ya hapo akashea na mashabiki wake lebo
yake hiyo mpya.
Tujikumbushe: Mapema mwaka jana kulitokea mikwaruzo kati ya Peter na Paul huku chanzo kikidaiwa Peter kuingilia ndoa ya Paul.
Bifu lao kubwa jingine ambalo lilikuwa la kimyakimya lilitokea tena
mwaka jana baada ya Peter kujitamba katika mitandao ya kijamii kuwa
amekuwa akitunga na kuimba nyimbo karibu zote za P-Square.
chanzo cha habari- globalpublishers.info

0 comments:
Post a Comment