Ujio Wa Zinadine Zidane, Hat-Trick Za Gareth Bale


zinedine zidane
January 9 ni siku ya mapumziko kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi, kwa sasa ni michuano mikubwa pekee kwa Tanzania inayoendelea, baada ya Ligi Kuu Tanzania bara kusimama ili kupisha michuano hiyo. Mtu wangu wa nguvu hiyo haimaanishi kuwa burudani ya soka ndio hiyo pekee.
1545
January 9 klabu ya Real Madrid ya Hispania ikiwa na kocha wake mpya Zinedine Zidane katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Hispania chini ya kocha huyo, imeibuka na ushindi wa jumla ya goli 5-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu.
4248
Real Madrid wakiwa na kocha wao huyo mpya, walionekana kujitahidi kucheza mchezo wa kuvutia na kufanikiwa kuvuna point tatu muhimu  kwa magoli ya Karim Benzema dakika ya 15, 90 na kufuatiwa na hat-trick ya Gareth Bale kwa kufunga goli tatu dakika ya 23, 49 na 63. Huu ni ushindi ambao tunaweza sema umemkaribisha Zidane Santiago Bernabeu.
2048

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment